Mark 12:35-37

Kristo Ni Mwana Wa Nani?

(Mathayo 22:41-46; Luka 20:41-44)

35 aYesu alipokuwa akifundisha Hekaluni, akauliza, “Imekuwaje walimu wa sheria wanasema kwamba Kristo
Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.
ni Mwana wa Daudi?
36 cKwa maana Daudi mwenyewe, akinena kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu, alisema:

“ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu:
“Keti mkono wangu wa kuume,
hadi nitakapowaweka adui zako
chini ya miguu yako.” ’
37 d Kwa hiyo Daudi mwenyewe anamwita ‘Bwana.’ Awezaje basi yeye kuwa mwanawe?”

Ule umati wote wa watu wakamsikiliza kwa furaha.

Copyright information for SwhNEN